Rais wa Marekani Joe Biden atatoa hotuba yake ya hali ya kitaifa kwenye kikao cha pamoja bunge Alhamisi usiku atajaribu kuelezea mafanikio ya utawala wake, kuwashinikiza wabunge kuchukua hatua juu ya msaada wa usalama na kuwashawishi wapiga kura kabla ya juhudi yake kutaka kuchaguliwa tena mwezi Novemba.
Biden alisema Jumatano katika video iliyobandikwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba alipanga kuelezea mapya juu ya maendeleo yetu na kueleza njia iliyo mbele.
Anatarajiwa kujadili mada kama vile miundombinu, bei ya dawa, deni la wanafunzi, haki za utoaji mimba na udhibiti wa bunduki.
Hotuba hiyo inajiri huku ikionekana kuna uwezekano mkubwa wa Biden kukabiliana na Rais wa zamani Donald Trump aliyekutana naye katika mpambano yao walipokutana katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2020.