Rais wa Iran, Ebrahim Raisi alisema Jumamosi kuwa Tehran ilikuwa makini katika mazungumzo yake ya nyuklia na mataifa yenye nguvu duniani mjini Vienna shirika rasmi la habari la IRNA liliripoti.
Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Marekani na Iran kufufua makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 yalianza tena Alhamis, katika mji mkuu wa Austria.
Wanadiplomasia kutoka Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Russia na China, wanasafiri kati ya pande hizo mbili kwa sababu Tehran inakataa kuwasiliana moja kwa moja na Washington. Chanzo kimoja cha ulaya kilizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, kilisema Ijumaa kwamba Iran imekubali kuendelea na mazungumzo kutoka pale walipoishia mwezi Juni. Maafisa wa Iran walikanusha hili.
Chini ya makubaliano ya awali ambayo Rais wa Marekani kwa wakati huo Donald Trump aliachana na mkataba mwaka 2018, Iran ilipunguza mpango wake wa nyuklia katika kurejesha ahueni kutoka kwa vikwazo vya Marekani, Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.