Rais wa Chad Mahamat Deby alisema uamuzi wa kusitisha mkataba wa kijeshi wa nchi hiyo na Ufaransa umechukuliwa kwa sababu umepitwa na wakati katika matamshi yake ya kwanza hadharani tangu kutangazwa kwa mshangao wiki iliyopita.
Katika hotuba aliyoitoa Jumapili jioni, Deby alisema mapatano hayo hayaambatani tena na usalama wa Chad au mahitaji ya kisiasa ya kijiografia. Chad imekuwa ikipambana na waasi wa jihadi kwa zaidi ya muongo mmoja, na kuungwa mkono na wanajeshi wa Ufaransa na Marekani kumeshindwa kuleta utulivu.
Hadi hivi karibuni nchi za Magharibi ziliichukulia Chad kama mshirika muhimu katika vita dhidi ya wanajihadi katika eneo la Sahel. Makundi yenye uhusiano na Boko Haram na Islamic State yanafanya kazi katika eneo la Ziwa Chad katika mpaka wake wa kusini magharibi.