Rais Vladimir Putin ameapa kuwapatia wa Russia ushindi kamili wakati wa sherehe ya kuapishwa kwake kwa mhula wa tano akiwa na madaraka zaidi kuliko hapo mwanzoni.
Putin hata hivyo alikiri kwamba Russia inakabiliwa na wakati mgumu akizungumzia vikazo vya nchi za magharibi ambvyo nchi hiyo haijapata kushuhudia kwa kuanzisha vita na Ukraine karibu miaka miwili ilyopita.
Kiongozi huyo wa Kremlin mwenye umri wa miaka 71 aliyetawala Russia tangu mwanzoni mwa karne hii alipata ushindi kwa mhula wa miaka 6 wakati wa uchaguzi wa rais wa mwezi March bila ya upinzani wowote.
Nchi za Ulaya zilitangaza mapema kwamba hawatapeleka wawakilishi wao kwenye sherehe hiyo iliyojumuisha gwaride la kijeshi na ibada kwenye kanisa la dhehebu ya Orthodox.