Rais Trump kutoa hisia zake juu ya uamuzi wa Seneti

Wademokrat waanza mjadala wa hati mbili za kumwondoa madarakani Rais Trump

Wademokrat waanza mjadala wa hati mbili za kumwondoa madarakani Rais Trump

Rais wa Marekani Donald Trump anatazamiwa kuzungumza kwa mara ya kwanza Alhamisi kutoka White House juu ya kadhia ya kutopatikana na hatia na baraza la Seneti la Marekani Jumatano kutokana na mashtaka mawili yaliyoletwa na Baraza la Wawakilishi.

Maseneta waliopiga kura na kumfutilia mashtaka mawili ya utumiaji mbaya wa madaraka na kuzuia utaratibu wa kazi ya bunge yaliyofikishwa na wademokrats wa Baraza la Wawakilishi.

Rais Trump alionekana kuwa na furaha kutokana na jinsi alivyotangaza mipango yake kwenye ukurasa wake wa twitter Jumatano saa kadhaa baada ya uamuzi huo kutolewa.

Kufuatia mchakato uliodumu kwa takriban miezi minne, na ulioigawanya Marekani kwa misingi ya kisiasa, Jaji Mkuu wa Marekani John Roberts alitoa tamko kwamba kufuatia kura mbili zilizopigwa kwenye Seneti , Rais Trump hajapatikana na hatia.

Katika kura ya kwanza, Seneta Mrepublikan wa Jimbo la Uttah Mitt Romney amekuwa seneta wa kwanza katika historia ya Marekani, kupiga kura iliyokinzana na wabunge wenzake, akishirikiana na wademokrat katika suala lenye umuhimu mkubwa kama hilo.

Trump alikabiliwa na tuhuma za kukiuka katiba, kwa kushikilia msaada wa kifedha uliokuwa umeidhinishwa na bunge kuisaidia Ukraine.

Anadaiwa kufanya hivyo kwa ajili ya maslahi yake binafsi ya kuitaka nchi hiyo kumchunguza kwanza mpinzani wake wa kisiasa Joe Biden na mwanawe.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.