Rais wa Russia Vladimir Putin Ijumaa alichukua hatua ya kuongeza muda wa uongozi wake nchini Russia kwa miaka sita zaidi, akitangaza kuwania katika uchaguzi wa rais wa 2024.
Putin bado anaungwa mkono baada ya takriban robo karne madarakani, licha ya kuanzisha operesheni maalum ya kijeshi nchini Ukraine na kuhatarisha maelfu ya raia wake , kuchochea mashambulizi ya mara kwa mara ndani ya Russia , ikiwa ni pamoja na moja huko Kremlin yenyewe -- na kuharibu taswira yake.
Uasi uliotekelezwa kwa muda mfupi mnamo Juni wa kiongozi wa mamluki Yevgeny Prigozhin ulizua uvumi kwamba Putin anaweza kupoteza mshikamano wake au kwamba ungeharibu sifa zake za kuwa shujaa.
Lakini aliibuka bila makovu ya kudumu, na kifo cha Prigozhin katika ajali ya kushangaza ya ndege miezi miwili baadaye kiliimarisha maoni kwamba Putin alikuwa katika udhibiti kamili.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AP.