Rais wa Marekani Barack Obama anaongoza sherehe za siku ya Martin Luther King katika sikukuu ya kitaifa ya ku-enzi maisha ya kiongozi huyo wa haki za kiraia.
Bw. Obama na mke wake Michelle wameshiriki misa ya kumbukumbu Jumaatu hapa Washington,wakati ujumbe wa baraza la mawaziri la rais ulihudhuria matukio ya kumbu kumbu na kufanya kazi za huduma za jamii kote nchini.
Kituo cha King huko Atlanta kimeandaa zaidi ya wiki moja ya matukio kukiwa na shughuli mbali mbali, kazi za kujitolea na mipango ya huduma za jamii. Kituo hicho kinaelezea siku hii kuwa ya kujihusisha na shughuli za jamii na kutoa huduma siku ya kufanya kazi na sio kukaa nyumbani.
Dr. King alikuwa na umri wa miaka 39 alipofariki dunia baada ya kupigwa risasi Aprili 4,1969. Lakini urithi wake unaendelea mpaka leo.