Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema Jumamosi kwamba mashambulizi ya hivi karibuni ya anga dhidi ya waasi wenye mahusiano na kundi la Islamic State mashariki mwa Congo yana uwezekano yameuwa wanamgambo wengi akiwemo mtengeneza mabomu wao.
Taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais haikutoa maelezo kuhusu mashambulizi ya anga ya Septemba 16 yaliyolilenga kundi la Allied Democratic Forces au ADF,kundi lenye itikadi kali linaloshutumiwa kwa ghasia za mara kwa mara zinazowalenga raia kutoka kambi za mashariki mwa Congo.
Mashambulizi hayo ya anga yalilenga kambi nne za ADF zilizopo kati ya kilomita 100-150 kutoka mpaka wa Uganda, kwa mujibu wa taarifa ya rais Museveni.
Uganda na Congo zilianzisha operesheni za pamoja za kijeshi dhidi ya ADF mwaka 2021.