Rais mteule wa Taiwan Lai – Ching-te ameuambia ujumbe unaotembelea nchini kwake wa maafisa wa zamani wa Marekani kwamba anatarajia Marekani itaendelea kuiunga mkono Taiwan —
Lai ambaye anajulikana zaidi kwa jina lake la kiingereza William amesema utawala wake utaendelea kutetea amani na uthabiti katika eneo la taiwan.
Mgombea wa urais wa Chama tawala cha DPP alishinda katika uchaguzi wa Jumamosi, ataingia madarakani Mei 20.
Akionyesha kuiunga mkono serikiali , afisa mwandamizi wa Marekani alisema wiki iliyopita kwamba rais Joe Biden alipanga kutuma ujumbe usio rasmi katika kisiwa hicho kinachodaiwa na China kwamba ni himaya yake.
Hata hivyo serikali ya Taiwan imekanusha madai hayo ya Beijing.