Rais mteule wa Marekani Donald Trump atashiriki kwa njia ya mtandao mkutano wa kila mwaka wa Jukwaa la Uchumi Duniani mjini Davos siku chache baada ya kuapishwa kwake, rais wa baraza hilo amesema Jumanne.
Børge Brende, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Norway ambaye anaongoza shirika hilo lenye makao yake mjini Geneva, amesema kuwa Trump alihudhuria mara mbili mkutano wa wasomi katika biashara, serikali, na viongozi wengine wakati wa muhula wake wa kwanza.
“Siku ya Alhamisi mchana, atajiunga nasi kwa njia ya kidijitali, moja kwa moja kwa njia ya mtandao katika mazungumzo na washiriki wetu”, Brende aliwaambia waandishi wa habari leo Jumanne wakati akiwasilisha mpango wa siku tano ambao utaanza Jumatatu ambayo ni siku ya kuapishwa kwa Trump.
“Tunadhani huo utakuwa wakati maalum sana”, aliongeza hasa kusaidia kujifunza vipaumbele vya sera vya utawala wake.