Rais mteule wa Iran athibitisha msimamo wake dhidi ya Israel

Rais mteule wa Iran, Masoud Pezeshkian, amethibitisha tena msimamo wa nchi yake dhidi ya Israel Jumatatu, akisema vuguvugu la upinzani katika eneo lote halitaruhusu sera za uhalifu za Israel dhidi ya Wapalestina kuendelea.

“Jamhuri ya Kiislamu daima imekuwa ikiunga mkono wananchi wa eneo hilo dhidi ya utawala haramu wa msimamo mkali wa Kiyahudi,” Pezeshkian amesema katika ujumbe wake kwa Hassan Nasrallah, kiongozi wa kundi la Hezbollah la Lebanon linaloungwa mkono na Iran.

Maoni haya yalionyesha hakuna mabadiliko katika sera za kikanda za serikali inayokuja chini ya Pezeshkian mwenye msimamo wa wastani ambaye alimshinda mpinzani wake mwenye msimamo mkali katika uchaguzi wa marudio wa wiki iliyopita.

Waislamu wa madhehebu ya Shia, Hezbollah na Hamas wa Sunni wa Palestina ni sehemu ya makundi yanayoungwa mkono na Iran katika eneo linalojulikana kama Axis of Resistance.