Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi amekubali kushindwa katika uchaguzi wa urais, hatua ambayo inafikisha ukomo utawala wa miaka 58 wa chama kilicho madarakani kwa sasa, Botswana Democratic Party, na ambacho kimekuwa madarakani tangu nchi hiyo ilipopata uhuru kutoka kwa Uingereza miaka ya 1960.
Hatua ya Masisi kukubali kushindwa imejiri kabla ya matokeo rasmi kutangazwa. Chama chake kinashikilia nafasi ya nne katika uchaguzi wa bunge, ishara ya kukataliwa kabisa na wapiga kura.
Muungano wa vyama vya upinzani Umbrella for Democratic Change, unaongoza katika hesabu ya kura, na kuonyesha ishara ya mgombea wake, Duma Boko, kuwa rais mpya wa nchi hiyo ya kusini mwa Afrika, ambayo ni mojawapo ya nchi ambayo ni mzaishaji mkubwa wa madini ya almasi duniani.
Rais Masisi amesema kwamba amempigia simu Boko na kumwambia kwamba amekubali kushindwa. Ameongezea kwamba Boko ndiye rais mteule.
Matokeo rasmi yanatarajiwa baadaye hii leo Ijumaa.