Rais Kibaki kuchukua hatua dhidi ya ongezeko la bei za vyakula.

Rais Mwai Kibaki wa Kenya

Rais Mwai Kibaki amesema serikali yake itachukua hatua ya kukinga raia wake kutokana na athari za ongezeko la bei za vyakula.

Rais wa Kenya Mwai Kibaki amesema serikali yake inachukua hatua kuwakinga raia wake kutokana na athari za kuongezeka kwa bei za vyakula.

Akiongea huko Nairobi jumtano Rais Kibaki amesema anatambua kwa kiasi kikubwa ugumu wa maisha wanaokumbana nao raia wa kenya kwasababu ya ongezeko la bei.

Bw. Kibaki amesema hatua za kupunguza athari ni pamoja na kupunguzwa kwa ushuru wa baadhi ya bidhaa, kuweka mikakati ya kuongeza akiba ya nafaka na ongezeko la mipango ya unafuu wa chakula katika maeneo yaliokumbwa na ukame.