Kagame, ambaye alikuwa rais mwaka 2000, anastahili kuendelea kuhudumu kwa muongo mwingine baada ya marekebisho ya katiba ya mwaka 2015, ambayo yalibadilisha ukomo wa rais kuhudumu, ambapo ingemlazimu kuachia ngazi miaka miwili baadaye.
Aliulizwa katika mahojiano na jarida la Jeune Afrique lililochapishwa Jumanne kuhusu nia yake kugombea katika uchaguzi wa utakaofanyika mwakani.
"Nina furaha na imani ambayo Wanyarwanda wameonyesha kwangu. Nitawatumikia daima, kadri ya uwezo wangu. Ndiyo, mimi ni mgombea," alisema.
Kagame alishinda uchaguzi ambao muhula wake ulikuwa ni miaka saba uliofanyika mara ya mwisho Agosti 2017 kwa kupata asilimia 98.63 ya kura, kulingana na tume ya uchaguzi.
Kagame alipata sifa za kimataifa kwa kusimamia amani na ukuaji wa uchumi tangu kumalizika wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, ambapo inakadiriwa Watutsi 800,000 na Wahutu wenye msimamo wa wastani waliuawa.
Lakini rais huyo amekabiliwa na ukosoaji wa hali ya juu, kwa kile amabacho makundi ya haki za binadamu yanasema amekuwa akikandamiza upinzani wa kisiasa na kuzuia uhuru wa vyombo vya habari.
Kagame amekuwa akikanusha tuhuma hizo.
Marekani ilikosoa mabadiliko ya katiba mwaka 2015, ikisema Kagame anapaswa kuachia madaraka muda wake utakapomalizika na kuruhusu kizazi kipya cha viongozi kuingia.
Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la AFP