Rais Joe Biden atangaza dola milioni 150 kukabiliana na saratani

  • VOA News

Rais Joe Biden akizungumzia mpango wa Cancer Moonshot, New Orleans Louisiana, Agosti 13, 2024. Picha ya AFP

Rais wa Marekani Joe Biden Jumanne alitembelea kituo maarufu cha kutibu Cancer katika jimbo la Lousiana na kutangaza dola milioni 150 katika ufadhili wa utafiti kuelekea lengo la kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya saratani nchini Marekani.

Cancer Moonshot ni mpango ambao una maana kubwa kwa Biden. Yeye na mke wake Jill Biden waliumwa saratani ya ngozi. Mwaka 2015, saratani mbaya ya ubongo ilimuua mtoto wao mkubwa, Beau.

“Tunasonga mbele kwa haraka, Biden alisema akiuelezea mpango huo, ambao una lengo la kupunguza viwango vya vifo kutokana na saratani nchini Marekani kwa angalau nusu ifikapo 2047.”

Saratani ni chanzo cha pili kikuu cha vifo duniani. Taasisi ya kitaifa ya saratani inatabiri kuwa Wamarekani milioni 2 watapimwa ugonjwa huu mwaka huu, ambao unaweza kujidhihirisha kwenye viungo, mifupa, na damu na ambao unaonekana katika mamia ya aina tofauti.