Hatua hiyo inaweza kuwasadia Wademocrats wenzake kupata uungwaji mkono mkubwa katika uchaguzi wa katikati ya muhula wa mwezi Novemba, lakini baadhi ya wachumi wanasema huenda hatua hiyo ikachochea ongezeko la mfumuko wa bei, na baadhi ya Warepublican katika bunge wanahoji iwapo rais ana mamlaka ya kisheria ya kufuta deni hilo.
Kufutwa kwa deni hilo kutatoa mabilioni ya dola kwa matumizi mapya ya wanunuzi ambayo yanaweza kulenga ununuzi wa nyumba na gharama nyingine za juu, kulingana na wachumi ambao wamesema hatua hiyo itaongeza kasoro mpya katika vita dhidi ya mfumuko wa bei nchini.
“Hatua hizi ni kwa ajili ya familia zinazohitaji zaidi pesa hizo , watu wa tabaka la kati na wanaofanya kazi ambao waliathiriwa vikali wakati wa janga la Covid,” Biden amesema wakati wa hotuba yake katika White House.
Aliahidi kuwa hakuna familia zenye mapato ya juu ambazo zitanufaika na hatua hiyo, akijibu ukosoaji mkubwa wa mpango wake huo.