Rais Biden kufanya mazungumzo na viongozi wa Umoja wa Ulaya

Rais wa Marekani Joe Bidenakizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa NATO mjini Brussels, Belgium June 14, 2021.

Kupambana na janga la corona na mabadiliko ya hali ya hewa, na pia kufanya kazi pamoja katika biashara na maswala ya mambo ya nje, yapo juu kwenye ajenda Jumanne wakati Rais wa Marekani Joe Biden na viongozi wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels.

Katika taarifa zilizotolewa kabla ya mazungumzo hayo pande hizo mbili zilisema zitarejea kuelezea msaada wao kwa kituo cha COVAX ili kuhakikisha upatikanaji sawa wa chanjo za COVID-19, na kufanya kazi pamoja kuhamasisha ahueni ya ulimwengu kutokana na athari za kiuchumi za janga hilo. Walipanga pia kujadili juhudi za kulifanyia mageuzi Shirika la Afya Ulimwenguni -WHO.

Hayo yote mawili yalikuwa mada kuu katika mikutano ya G-7 na NATO wiki hii, Russia na China zitakuwa tena kwenye ajenda Jumanne.

Wote White House na Umoja wa Ulaya walisema viongozi hao pia wataelezea nia yao ya dhati kuunga mkono demokrasia na kupambana na ufisadi, na kusimamia haki za binadamu kote ulimwenguni. Wanaahidi pia kushirikiana katika maswala yanayohusu usalama wa mitandao na Uhamiaji.