Rais Biden kutangaza jinsi serikali kuu inajiandaa kukabiliana na ongezeko la kesi za Omicron.

Rais Biden alipozungumza katika mkutano wa demokrasia akiwa katika ikulu ya Marekani Desemba 10, 2021, in Washington. (AP Photo/Evan Vucci)

Rais wa Marekani Joe Biden anatazamiwa kuhutubia taifa Jumanne kutangaza jinsi serikali yake inajiandaa kukabiliana na ongezeko la idadi ya kesi za covid aina ya Omicron.

Rais wa Marekani Joe Biden anatazamiwa kuhutubia taifa Jumanne kutangaza jinsi serikali yake inajiandaa kukabiliana na ongezeko la idadi ya kesi za covid aina ya Omicron.

Kuongezeka kwa kesi hizo nchini Marekani kumesababisha baadhi ya vyuo vikuu kutangaza kwamba vimehama au vitahamia katika masomo kwa njia ya mtandao ikiwa ni pamoja na Harvard ambayo ilisema itahamishia masomo yake kwa njia hiyo kwa takriban wiki tatu za kwanza za Januari.

Huko barani Ulaya, kuongezeka kwa idadi ya kesi kumesababisha baadhi ya serikali kutaka masharti yarejeshwe tena wakikukumbushia kufungwa kwa shughuli kutokana na COVID mapema mwaka huu.

Uholanzi inafunga tena shughuli, Waziri Mkuu Mark Rutte alisema Jumamosi katika hotuba kwa njia ya televisheni. Hatua hizo mpya, kuanzia Jumapili, Rutte alisema, ni kwa sababu ya wimbi la tano la COVID-19, kwa sababu ya aina ya omicron inayoambukiza kwa kasi kubwa.

Kwa mujibu wa kanuni mpya, maduka yote yasiyo ya lazima yatafungwa walau hadi katikati ya Januari. Wageni wawili tu ndio wataruhusiwa kutembee kwenye nyumba ya mtu kwa wakati mmoja. Wageni wanne, hata hivyo, wataruhusiwa wakati wa sikukuu zijazo kutanzia Desemba 24 - 26 na wakati wa mkesha wa Mwaka Mpya na Siku ya Mwaka Mpya.

Shule zitafungwa mara moja mpaka Januari 9.