Rais Biden, atoa msamaha kwa Marcus Garvey, baada ya kupita miaka mingi

Rais wa Marekani, Joe Biden, Jumapili amemsamehe mzalendo mweusi Marcus Garvey, ambaye alimshawishi Malcolm X na viongozi wengine wa haki za kiraia ambaye alipatikana na hatia ya ulaghai wa barua katika miaka ya 1920.

Pia waliopokea msamaha walikuwa ni mbunge mwandamizi wa Virginia na mawakili wa haki za wahamiaji, mageuzi ya haki ya jinai na kuzuia ghasia za bunduki.

Viongozi wa bunge walikuwa wameshinikiza Biden amsamehe Garvey, huku wafuasi wakisema kwamba hukumu ya Garvey ilichochewa kisiasa na juhudi za kumnyamazisha kiongozi huyo anayezidi kupendwa na watu wengi ambaye alizungumza juu ya kiburi cha rangi.

Baada ya Garvey kuhukumiwa, alifukuzwa na kurejeshwa Jamaica, ambako alizaliwa. Alikufa mwaka 1940.

Martin Luther King Jr. alisema kuhusu Garvey, “alikuwa mtu wa kwanza, wa kiwango cha juu na kuwapa mamilioni ya watu Weusi hisia za utu na hatima zao.

Haijabainika iwapo Rais Biden, ambaye ataondoka madarakani Jumatatu, atawasamehe watu ambao wameshutumiwa au kutishiwa na Rais mteule Donald Trump.