Rais Biden atoa matumaini kwa wananchi kuelekea kuishinda COVID-19

Rais Joe Biden

Rais Joe Biden amezungumza kwa tahadhari juu ya matumaini ya hali ya mambo kubadilika kutokana na juhudi za kupambana na janga la virusi vya Corona alipo lihutubia taifa kwa mara ya kwanza jana usiku.

Biden alikuwa amezungumzia juu ya athari na maafa yaliyotokea Marekani mwaka mmoja kamili tangu ugonjwa wa COVID-19 kutangazwa na kuwataka Wamarekani kusaidia katika kukabiliana na changamoto za siku zijazo.

Ni mwaka mmoja tangu Shirika la Afya Duniani, WHO, kutangaza COVID-19 ni janga la dunia na tangu wakati huo zaidi ya watu milioni 2 laki sita wamefariki kote duninani na kati ya hao laki tano elfu 30 wamefarki Marekani. Rais Biden alizungumzia maafa yaliyo likumba taifa zima.

Rais Biden ameeleza : "Sote tumepoteza kitu fulani. Ni kutabika kwa pamoja, ni kujito mhanga kwa pamja, ni mwaka ulokua na vifo vingi na sote kupoteza namna tulivyokua tunaishi."

Katika hotuba yake ya kwanza, ikiwa ni siku 50 tangu kuchukua madaraka Rais Joe BIden alifafanua hatua utawala wake unachukua kuvishinda virusi hivyo vya hatari, ikiwa ni pamoja na kuvuka malengo yake ya kuwapa chanjo watu milioni 100 mnamo siku 100 za kwanza za utawala wake.

Rais amesema : "Kwa hakika tuko katika njia iliyo sawa, kufikia lengo la kuwapa chanjo watu milioni 100 ifikapo siku ya 60 ya utawala wangu. Hakuna nchi duniani iliyofanya hivyo."

Biden anasema ana agizia majimbo yote kuwezesha wamarekani wote kuanza kupata chanjo kuanzia May Mosi. Lakini anakabiliwa na changamoto kadhaa, ikiwa ni pamoja na wale wanaosita kupinga chanjo hiyo na serikali za baadhi ya majimbo zinazopuzi muongozo wa afya wa kitaifa."

"Hii Barakoa. Chombo rahisi kabisa kuokoa maisha. Ndio kitu kinacho tugombanisha, majimbo yakigombana kati yao badala ya kufanya kazi kwa pamoja. Haya ni mambo yanayo bidi kusitishwa," ameongeza.

Wachambuzi wamegawika kuhusiana na chanjo na masharti ya afya yanasababisha mivutano ya kisiasa hasa mnamo siku za mwanzoni za kuanza janga hili, anasema Katherine Baicker wa Chuo Kikuu cha Chicago.

Baicker anaeleza : "Watu wamekua wakipata maelezo yanayotatanisha kuhusu afya ya umaa, na mazingira yamesababisha mivutano lkufikia kiwango ambacho watu hawana tena Imani na ujumbe wa kisayansi kuhusu afya ya uma. Kwa hakika inafahamika kichukulia maagizo yanayo kinzana watu wanayosikia, na nina dhani ni moja wapo ya madhara ya kudumu yaliyokwisha tendeka."

Kabla ya kutoa hotuba hiyo Biden alitia sani mswaada wa sheria wa kuunusuru uchumi na kupambana na janga la COVID-19 utakao gharimu dola trilioni 1.9.