Baraza la Seneti la Marekani mapema Jumamosi asubuhi limepitisha mswada wa bajeti kuifadhili serikali kuu ya Marekani hadi mwezi Machi mwakani.
Mabaraza mawili ya bunge yalipitisha mswada huo kuepuka kufungwa kwa serikali.
Rais Joe Biden Jumamosi amesaini mswada huo kuwa sheria.
Mswada huo wa sheria utaifadhili serikali hadi mwezi Machi na umetenga dola bilioni 100 kwa ajili ya majanga na msaada wa dola bilioni 10 kwa wakulima. Hautaongeza kiwango cha kukopa madeni.
Baraza la Seneti limepitisha mswada huo kwa kura 85 dhidi ya 11 baada ya Baraza la wawakilishi kuupitisha kwa kura 366 dhidi ya 34, baada ya kujaribu mara mbili bila mafanikio.
Kura 34 za kupinga mswada huo zote zilikuwa za Warepublican.