Rais Biden aonya watu kuwa waangalifu dhidi ya virusi vya Monkeypox

Rais Joe Biden akilakiwa na balozi wa Marekani Japan Rahm Emmanuel na waziri wa mambo ya nje wa Japan Yoshimasa Hayashi alipowasili katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Yokota huko Fussa Mei 22,2022, REUTERS/Jonathan Ernst

Virusi vya Monkeypox vimevuta hisia za Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye alisema Jumapili kwamba watu wanapaswa kuwa waangalifu dhidi ya ugonjwa huo ambao una uwezekano wa athari mbaya ikiwa utaenea zaidi.

Virusi vya Monkeypox vimevuta hisia za Rais wa Marekani Joe Biden, ambaye alisema Jumapili kwamba watu wanapaswa kuwa waangalifu dhidi ya ugonjwa huo ambao una uwezekano wa athari mbaya ikiwa utaenea zaidi.

Kesi kadhaa za monkey pox zimegunduliwa Amerika Kaskazini na Ulaya tangu mapema mwezi Mei, na kuzua wasiwasi kwa ugonjwa huo, ambao umeenea katika sehemu za Afrika.

Kiongozi huyo wa Marekani, katika safari yake ya kwanza ya Asia kama rais, alisema mjini Seoul kwamba maafisa wa afya hawajamweleza kikamilifu kuhusu kiwango cha Mmaambukizi nchini Marekani.

Lakini ni jambo ambalo kila mtu anapaswa kuwa na wasiwasi nalo, Biden aliwaambia waandishi wa habari kabla ya kupanda ndege yake Air Force One kuelekea Tokyo.

"Tunalifanyia kazi kwa bidii kujua tunachofanya na ni chanjo gani ikiwa inapatikana kwa hiyo." Aliongeza.

Kumekuwa na maelfu ya maambukizi ya wanadamu katika sehemu za Afrika ya Kati na Magharibi katika miaka ya hivi karibuni lakini ni nadra katika Ulaya na Amerika Kaskazini.