Rais Biden anatarajiwa kukutana wa wademocrat kutangaza makubaliano ya dola Trilioni 3.5

Rais wa Marekani, Joe Biden

Mpango huo utasaidia kupanua matumizi ya huduma za afya kwa wazee, mabadiliko ya hali ya hewa na mipango ya kuzisaidia familia, kiongozi wa waliowengi Chuck Schuma alisema.

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kwenda bungeni Jumatano kukutana na wademocrats katika baraza la seneti baada ya wabunge kutangaza makubaliano juu ya mpango wa dola trilioni 3.5 za kupanua matumizi ya huduma za afya kwa wazee, mabadiliko ya hali ya hewa na mipango ya kuzisaidia familia, kiongozi wa waliowengi Chuck Schuma alisema.

Mpango huo utakuwa uwekezaji mkubwa zaidi kwa miongo kadhaa katika familia za daraja la kati, Schumer alisema Jumanne. Wakati huo huo, seneta Mark Warner m-Democrat kutoka jimbo la Virginia aliwaambia waandishi wa habari kwamba mpango huo ulijumuisha vifungu ambavyo vitagharamia kikamilifu gharama za program hizo. Wakati Warner hakuelezea namna hatua hiyo itakavyolipwa Biden anashinikiza ongezeko la kodi kwa matajiri na kwenye mashirika.

Wa-Republican katika bunge wanapinga ongezeko la kodi, baada ya kufanikiwa kupunguzwa kwa kodi ikiwemo kiwango cha kodi kwenye mashirika wakati wa utawala uliopita wa Rais Donald Trump.