Rais Biden ametia saini kuwa sheria siku ya kumalizika utumwa Marekani

Rais Biden akitia saini kuwa sheria sikukuu ya Juneteenth

Juneteenth National Independence Day itakuwa inaadhimishwa Juni 19 ya kila mwaka. Ni siku katika mwaka 1865 wakati wanajeshi wa muungano walipoliarifu kundi la watumwa weusi kwenye jimbo la Texas juu ya uhuru wao miaka miwili na nusu baada ya Rais Abraham Lincoln kutia saini tangazo la ukombozi

Rais wa Marekani Joe Biden ametia saini kuwa sharia hapo Alhamis kubuniwa kwa sikukuu mpya ya serikali kuu inayokumbuka kumalizika kwa utumwa nchini Marekani.

Juneteenth National Independence Day itakuwa inaadhimishwa Juni 19 ya kila mwaka. Kwa kufanya Juneteenth kuwa sikukuu ya serikali kuu wamarekani wote wanaweza kuhisi nguvu ya siku hii na kujifunza kutoka kwenye historia yetu na kusheherekea maendeleo na kukabiliana na umbali ambao tumefika, na umbali ambao tunapaswa kusafiri, Biden alisema.

Sikukuu hii inaadhimisha siku katika mwaka 1865 wakati wanajeshi wa muungano walipoliarifu kundi la watumwa weusi huko Galveston kwenye jimbo la Texas juu ya uhuru wao miaka miwili na nusu baada ya Rais Abraham Lincoln kutia saini tangazo la ukombozi.