Rais wa Marekani, Joe Biden ameishutumu sheria mpya ya Uganda ya kukabiliana na wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja akita yenye kutia aibu na ukiukwaji mbaya wa haki sawa za binadamu nchini Uganda.
Katika taarifa ya Jumatatu, rais Biden amesema sheria hiyo ndilo tukio la hivi karibuni katika hali inayotia mashaka ya ukiukwaji wa haki za binadamu na rushwa nchini Uganda.
Amesema Marekani itafanya tathimini ya athari za sheria hiyo katika nyanja zote za ushirikiano wa Marekani na Uganda, na kusema inaweza ikasababisha kuwekewa vikwazo kwa baadhi ya watu.
“Tunafikiria njia nyingine zaidi, ikijumuisha kuandaliwa kwa vikwazo, na marufuku za kuingia Marekani dhidi ya mtu yoyote aliyehusika katika uvunjwaji mbaya wa haki za binadamu ama rushwa,” rais Biden alisema.
Wanajumuiya wa wanao shiriki mapenzi ya jinsia moja wa Uganda wamekubwa na mshituko kufuatia kupitishwa kwa sheria ya kukabiliana na wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.