Rais Joe Biden, anaomba karibu dola bilioni 100 za msaada wa dharura wa maafa baada ya vimbunga Helene na Milton, na majanga mengine ya asili, akiwaambia wabunge pesa hizo zinahitajika haraka.
Barua ya Jumatatu kwa Spika wa Bunge, Mike Johnson imeandikwa wakati wabunge wanakutana wakati wa kikao mwishoni kumaliza vipaumbele muhimu kabla ya kutoa nafasi kwa bunge jipya na utawala unaokuja wa Rais mteuleTrump.
Rais Biden amesema amekutana moja kwa moja na wale walioathiriwa na dhoruba na alisikia kile wakaazi na wafanyabiashara wanahitaji kutoka kwa serikali kuu.
Sehemu kubwa zaidi ya pesa hizo, takriban dola bilioni 40, zingeenda hazina kuu ya misaada ya maafa kwenye idara kudhibiti dharura FEMA.
Biden amesema hazina hiyo itakabiliwa na upungufu kwa mwaka huu wa bajeti bila kuwa na pesa za ziada.