Hasan Abdalla aliteuliwa kwa mara ya kwanza Agosti 2022 baada ya kujiuzulu ghafla kwa Tarek Amer
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi ameongeza muda wa kuhudumu kaimu gavana wa benki kuu, Hasan Abdalla kwa mwaka wa tatu, gazeti rasmi lilisema leo Jumatatu.
Abdalla ambaye kwa miaka 16 alikuwa mkuu wa benki ya kimataifa kwa nchi za kiarabu na Afrika yenye makao yake mjini Cairo, aliteuliwa kwa mara ya kwanza Agosti mwaka 2022 baada ya kujiuzulu ghafla kwa Tarek Amer aliyehudumu kwa muda mrefu kwenye nafasi hiyo. Uteuzi wa Abdalla uliongezewa muda mwaka 2023.