Hatuahii imekuja baada ya Rais William Ruto kuhutubia taifa na kumtaka Odinga kusitisha mandamano ya wafuasi wake.
Rais Ruto, ambaye alikuwa akihutubia taifa kutoka Ikulu ya Nairobi, alitoa wito wa kuwepo kwa ushirikiano wa pande mbili Bungeni kuhusu kuundwa upya kwa Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi (IEBC), mojawapo ya masuala muhimu yaliyochangia mwito wa Azimio wa maandamano nchini kote kupinga serikali.
"Ninapendekeza ushirikiano wa pande mbili Bungeni kuhusu uundaji upya wa jopo la IEBC ndani ya vigezo vya sheria na katiba'" akasema.
Kwa Upande wake Raila amesema wameamua kusitisha maandamano ya Jumatatu na Alhamisi wiki hii ili kuruhusu mazungumzo kuhusu masuala yaliyoibuliwa.
"Tuko tayari kushiriki na tutajihusisha bila aina yoyote ya rushwa na mchakato huu unapaswa kuanza mapema kesho."
Odinga pamoja na viongozi wa Azimio waliibua maswala mazito ikiwa ni pamoja na gharama ya maisha , suala la uteuzi wa makamishana wa IEBC , ukosefu wa uwazi katika mfumo wa uchaguzi, na vilevile idara ya usalama kutumia nguvu kupita kiasi katika kukabili wanadamanji.
Maandamano ya wiki jana yalikumbwa na makabaliano makali baina ya maafisa wa usalama na waandamanji huku takriban watu 10 wakiwemo maafisa wa polisi wakipoteza maisha.
Wakenya wamepongeza hatua ya Rais William Ruto na Kinara wa ODM Odinga , kwa kuzika tofauti zao kando ilikutoa nafasi kwa mazungumzo.
Awali viongozi wa kidini waliwahimiza vinara hao wawili kusitisha uhasama baina yao kwani mgogoro baina yao uliiweka taifa katika hatari Zaidi.
Mazungumzo haya aidha yanajiri wakati ambapo mabalozi kutoka mataifa ya nje ikiwemo Marekani kushinikiza wawili hao kufanya mazungmzo.
Kwa sasa ni afueni kubwa kwa wafanya biashara waliokuwa wakipoteza mabilioni ya fedha kila wakati maandamano yanapofanyika na vile vile kwa wafunzi ambao masomo yao yalikuwa yametatizwa.