Ureno inafanya uchaguzi mkuu leo Jumapili huku kukiwa na kashfa za rushwa na hali ngumu ya uchumi ambayo imeharibu imani katika vyama vyenye msimamo wa wastani na unaweza kuwasukuma idadi kubwa ya wapiga kura katika mikono ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia.
Kashfa za karibuni kuhusu ufisadi zimevitia doa vyama viwili ambavyo vimekuwa madarakani kwa kupishana kwa miongo kadhaa, chama cha mrengo wa kushoto cha Socialist Party, na kile cha mrengo wa kati kulia Social Democratic Party ambacho kiko katika ushindani kikiwa na ushirika na vyama viwili vidogo katika muungano uitwao Democratic Alliance.
Vyama hivyo vya kiasili bado vinatarajiwa kukusanya kura nyingi. Umma kuchanganyikiwa na siasa ni kama kawaida tayari kumeibuka vilio juu ya rushwa.
Mishahara midogo na gharama kubwa ya maisha vilikuwa vibaya sana mwaka jana kwa kuongezeka kwa mfumuko wa bei na viwango vya riba, pamoja na mgogoro wa makazi na utoaji mbaya huduma za afya ya umma vilichangia watu kutoridhishwa.