Takriban raia watatu wa Palestina wameuwawa katika mashambulizi kadhaa ya Israel katika upande wa kusini wa ukanda wa Gaza, maafisa wamesema Jumamosi, licha ya kuwepo kwa maandalizi ya mazungumzo ya hali ya juu ya kusitisha mapigano katika jiji kuu la Misri.
Miongoni mwa waliofariki dunia walikuwemo watu 11 wa familia moja ikijumuisha watoto wawili, baada ya shambulizi la anga la Israel kulenga nyumba yao katika mji wa Khan Younis, mapema Jumamosi, kwa mujibu wa Hospitali ya Nasser, ambapo maiti na waliojeruhiwa hupelekwa.
Hospitali hiyo ilipokea jumla ya maiti 33 ambao waliuwawa katika mashambulizi matatu tofauti, na kuzunguka Khan Younis.
Hospitali ya mji ya Al-Aqsa Martyrs imesema ilipokea maiti wengine watatu kutoka katika mashambulizi ya mapema Jumamosi.
17 wengine waliuwawa baada ya shambulizi la barabarani kusini mwa Khan Younis ikijumuisha abiria wa pikipiki kwa mujibu wa hospitali hiyo.