Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini China wanafuatilia uchaguzi mkuu wa Marekani kwa kuandika jumbe za kejeli hasa baada ya rais Donald Trump kudai kwamba alikuwa anaongoza katika hesabu ya kura.
Wameandika kwamba hatua ya rais Trump ni sawa na kujitangaza mshindi kabla ya mashindano kukamilika.
Wakati raia wa China wanakejeli rais Donald Trump, izingatiwe kwamba viongozi wa chama cha Kikomunisti, kinachotawala nchini China, huchaguliwa katika mchakato wa siri na ambao huhudhuriwa na wanachama pekee.
Uhusiano kati ya China na Marekani umekuwa mbaya katika utawala wa rais Donald Trump hasa kuhusu hati miliki za kiteknolojia, biashara na Hong Kong, Pamoja na janga la virusi vya Corona.
Utawala wa rais Trump imeiwekea China vikwazo kadhaa vya Kiuchumi.