Raia wa Cape Verde wanapiga kura leo kuchagua rais ajaye

Jorge Carlos Fonseca, Rais wa Cape Verde

Wagombea saba wanawania kuchukua nafasi ya Jorge Carlos Fonseca lakini ni wawili pekee wanaofikiriwa kuwa wagombea wenye ushawishi mkubwa Carlos Veiga kutoka chama cha mrengo wa kati cha Fonseca cha Movement for Democracy na Jose Maria Neves wa chama cha mrengo wa kushoto cha PAICV

Nchi kwenye visiwa vya Afrika magharibi ya Cape Verde moja yenye demokrasia thabiti barani humo ilipiga kura Jumapili kwa rais mpya ambaye atakuwa na jukumu la kushughulikia uchumi wake unaosukumwa na utalii ambao ulianguka baada ya janga la COVID-19.

Wagombea saba wanawania kuchukua nafasi ya Jorge Carlos Fonseca lakini ni wawili pekee wanaofikiriwa kuwa wagombea wenye ushawishi mkubwa, Carlos Veiga kutoka chama cha mrengo wa kati cha Fonseca, cha Movement for Democracy (MpD) na Jose Maria Neves, wa chama cha mrengo wa kushoto, cha African Party for the Independence of Cape Verde (PAICV).

Wote wawili ni mawaziri wakuu wa zamani. Veiga mwenye umri wa miaka 72 aliwahi kuhudumu kutoka mwaka 1991 hadi 2000, na Neves mwenye miaka 61 alihudumu kutoka 2001 hadi 2016.