Putin kukutana na kiongozi wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei mjini Tehran,Jumanne

Rais wa Russia Vladimir Putin na kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, mjini,Tehran kwenye picha ya maktaba

Rais wa Russia Vladimir Pitin Jumanne anaitembelea Tehran, Iran kwa mkutano na kiongozi wa taifa hilo Ayatollah Ali Khamenei ikiwa ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu kufanyika kwa uvamizi nchini Ukraine.

Putin anakabiliwa na vikwazo vikali zaidi kutoka kwa mataifa ya magharibi kutokana na uvamizi huo, wakati akigeukia mataifa kama vile China , Iran na India. Putin anazuru Tehran siku 3 baada ya rais wa Marekani Joe Biden kukamilisha ziara yake ya mashariki ya kati iliyompeleka hadi Saudi Arabia.

Ziara hiyo ni ya tano ya kikao chake na kiongozi mkuu wa pili wa Iran aliyeingia madarakani ,mwaka wa 1989. Mshauri wa sera za mambo ya nje wa Putin Yuri Ushakov amewaambia wanahabari mjini Moscow kwamba ziara yake nchini Iran ni muhumu sana, wakati viongozi hao wakitarajiwa kushauriana uhusiano kati ya mataifa yote mawili pamoja na masuala mengine ya kimataifa.