Putin atakosa kuhudhuria kongamano hilo kama hatua ya kuzuia majibizano kati ya Marekani na washirika wake kuhusu vita vinavyoendelea nchini Ukraine.
Afisa anayesimamia maandalizi ya kongamano hilo, Luhut Binsar Pandjaitan, amesema kwamba hatua ya Putin kuamia kutohudhuria ni nzuri kwa washirika wote.
"Ni rasmi kwamba rais Vladimir Putin hatahudhuria kongamano la nchi 20 tajiri duniani na anatawakilishwa na afisa wa ngazi ya juu. Hili limejadiliwa katika mazungumzo ya simu kati ya rais Joko Widodo na Putin. Rais Widodo ambaye ni kiongozi wa sasa wa G20, anataka kujali maslahi ya kila mtu kwa kuwasiliana na viongozi wengine kwa maslahi yetu sote."
Rais wa Marekani Joe Biden, Xi Jinping wa China na viongozi wengine wa dunia wanatarajiwa kuhudhiria kongamano hilo litakaloanza Novemba 15.
Kongamano hilo lingekuwa la kwanza kuwakutanisha Biden na Putin tangu Russia ilipovamia Ukraine kijeshi, Februari mwaka huu.
Kongamano hilo litafanyika kwenye kisiwa cha Bali, chini ya mwenyekiti Joko Widodo.