Matokeo ya awali nchini Russia yanasema rais Vladimir Putin ameshinda muhula wanne madarakani kwa zaidi ya asilimia 75 za kura zilizopigwa.
Awali kura ya maoni ilionyesha kuwa Putin alikuwa anaungwa mkono zaidi kuliko wapinzani wake wote .
Putin amekuwa katika nafasi ya uongozi Rashia kwa miaka ipatayo 18.
Akizungumza na maelfu ya watu huko Manezhnaya Square karibu na Kremlin Jumapili usiku aliwasifu wale waliompigia kura kama timu kubwa ya taifa akisema kwamba sisi tunaelekea kwenye mafanikio.
Alipoulizwa kama atagombea tena 2030 kiongozi huyo wa Rashia mwenye umri wa maiak 65 alijibu kwa ukali, huu ni ujinga unafikiri ntakaa hapa mpaka nikiwa na miaka 100?
Putin alishindana na wapinzani 7 lakini hakuna hata mmoja aliyekuwa tishio la kweli. Kila mmoja wa wagombea hao akiwamo mcheza filamu nyota wa hali halisi ya maisha na mpenda uzawa kupindukia kati yao walitarajiwa kupata kura chache sana.
Uchaguzi wa Jumapili unafanyika katika nyakati 11 tofauti, ukianza na mashariki ya mbali na kumalizika na wilaya ya Kaliningrad. Takriban watu milioni 109 wameandikishwa kupiga kura. Shirika la serikali linaloendesha uchaguzi lilisema linatarajia asilimia 71 ya watu hao waliojiandikisha kuja kupiga kura.
Ingawaje, Kituo cha kitafiti cha shirika la kiraia Levada kimefanya utafiti Disemba 2017 na utafiti huo unaonyesha asilimia 58 ya wapiga kura walikuwa wamepanga kususia uchaguzi huo.
Hasimu wa Putin kisiasa ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani Alexei Navalny aliyekuwa ni tishio kubwa kwa Putin ametolewa katika kinyang’anyiro hicho cha urais baada ya kukutwa na hatia ya ubadhirifu Disemba 2017.
Baada ya kupewa kifungo mbadala cha miaka mitano, amesema kuwa hukumu hiyo ya mahakama ilikuwa inamsukumo wa kisiasa, ili kumuondoa katika mbio hizo za uchaguzi.
Navalny anaongoza juhudi za kususia uchaguzi, wakati waandaaji wa uchaguzi wa Urusi wanategemea wapiga kura wengi zaidi kuhalalisha uchaguzi ambao kwa muda mrefu unadaiwa umeshaamuliwa.