Rais wa Russia Vladimir Putin amefanya mazungumzo na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, ambaye pia ni rais wa Senegal Macky Sall na kuzungumzia namna ya kuhakikisha kwamba nafaka kutoka Ukraine zinafika katika masoko ya kimataifa.
Kulingana na umoja wa mataifa, mataifa ya Afrika yaliagiza asilimia 44 ya ngano kutoka Russia na Ukraine kati yam waka 2018 na 2020.
Kulingana na benki ya maendeleo Afrika, bei ya ngano imepanda kwa asilimia 45 kote duniani kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.
Russia, ambayo ni mzalishaji mkubwa wa ngano kote duniani, imeyataka mataifa ya magharibi kuondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi yake ndipo iruhusu nafaka kusafirishwa hadi masoko ya kimataifa.
Japo vikwazo havilengi chakula na mbolea, kampuni za kimataifa zinazosafirisha mizigo zimesita kusafirisha bidhaa za Russia.