Rais wa Russia Vladimir Putin ameunga mkono pendekezo la Marekani la kusitisha vita kati ya Russia na Ukraine lakini amesisitiza umuhimu wa kufanyia kazi maelezo yaliyomo katika pendekezo hilo.
“Tunakubaliana na mapendekezo ya kusitisha mapigano, lakini tunaendelea kuhisi kwamba sitisho la mapigano litaleta amani ya kudumu na kuondoa mizizi ya mgogoro huu,” Putin aliwaambia waandishi wa habari Alhamisi mjini Moscow.
“Pengine nitampigia simu Rais Trump na nifanye nae mazungumzo,” alisema.
Akiwa White House, Trump alisema “itavunja moyo sana” ikiwa Russia itaamua kukataa juhudi za Marekani za kumaliza mapigano.
“Tunapendelea kuona sitisho la mapigano kutoka kwa Russia,” Trump aliwambia waandishi wa habari. Maelezo mengi kuhusu makubaliano kamili yamejadiliwa. Sasa tutaona kama Russia inakubali au haiukubali, ikipinga, litakuwa jambo la kuvunja moyo sana kwa ulimwengu.”