Alipoulizwa kuhusu mpango wake wa mashambulizi ya kijeshi ndani ya Ukraine, Putin alisema kwamba, wanajeshi wa Ukraine wanahitaji kusukumwa nyuma, kiasi kwamba silaha za masafa marefu kutoka magharibi zinazotumiwa na Ukraine, hazitaweza kufikia miji yenye amani ndani ya Russia. Aliongeza kusema kwamba kwa muda wote huu, jeshi lake limekuwa likitekeleza hilo.
Ukraine katika siku za karibuni imefanya mashambulizi ndani ya Russia, likiwemo lile la Desemba 30 kwenye mji wa mpakani wa Belgorod, lililouwa watu 25 na kujeruhi wengine zaidi ya 100. Putin pia ameongeza kusema kwamba wachunguzi wamedhibitisha kwamba Ukraine ilitumia mfumo wa ulinzi wa anga aina ya Patriot kutoka Marekani, kuangusha ndege ya kijeshi karibu na Belgorod, hapo Januari 24.