Rais Obama aitembelea Kenya (1)
Rais Barack Obama awasili kwa mkutano na masuala ya uhusiano na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwenye ikulu, Jumamosi, Julai 25, mjini Nairobi, Kenya. Ziara ya Obama imelenga masuala ya biashara na uchumi, pamoja na usalama na kukabiliana na ugaidi.
Rais wa Marekani, Barack Obama anakagua gwaride baada ya kuwasili na kulakiwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwenye Ikulu mjini Nairobi, Jumamosi, Julai 25, 2015. Rais Obama amesema bara la Afrika liko katika mbio, wakati akiwa kwenye ziara ya Kenya, katika taifa la Afrika Mashariki ambalo ana uhusiano mkubwa wa kifamilia na rais huyo wa Marekani.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kulia, akiangalia huku Rais Barack Obama, katikati akimkubatia dada yake wa kambo, Auma Obama mara baada ya kuwasili kwenye uwanya wa ndege wa kimataifa wa Kenyatta, Ijumaa, Julai 24, 2015. Obama anayatembelea mataifa mawili ya Afrika ambako atakuwa ni rais wa kwanza wa Marekani aliye madarakani kuitembelea Kenya na Ethiopia.
Rais wa Marekani, Barack Obama anakagua gwaride baada ya kuwasili na kulakiwa na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwenye Ikulu mjini Nairobi, Jumamosi, Julai 25, 2015. Rais Obama amesema bara la Afrika liko katika mbio, wakati akiwa kwenye ziara ya Kenya, katika taifa la Afrika Mashariki ambalo ana uhusiano mkubwa wa kifamilia na rais huyo wa Marekani.
Rais Barack Obama anaangalia maonyesho ya nishati ya jua alipotembelea Power Africa Innovation Fair, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi. Ziara ya Obama nchini Kenya imelenga kwenye masuala ya biashara na uchumi, pamoja na usalama na ushirikiano wa kukabiliana na ugaidi.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anaongea wakati wa mkutano wa pamoja na Rais Barack Obama kwenye ikulu, Jumamosi, Julai 25, 2015, huko Nairobi, Kenya. Obama amelitaja bara la Afrika kuwa linasonga mbele.
Rais Barack Obama, kushoto, na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wakiwapungia watu wakati wakiondoka kwenye mkutano wa kimataifa wa ujasiriamali kwenye jengo la Umoja wa mataifa, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi. Ziara ya Obama Kenya imelenga kwenye masuala ya biashara na uchumi, pamoja na usalama na ushirikiano katika kukabiliana na ugaidi.
Rais Barack Obama anaangalia jinsi ya kufanya malipo kwa njia ya simu ya mkononi na matumizi ya nishati ya nguvu za jua wakati wa maonyesho ya Power Africa Innovation Fair, Jumamosi, Julai 25, 2015 mjini Nairobi. ziara ya Obama Kenya imelenga masuala ya biashara na uchumi, pamoja na usalama na ushirikiano katika kukabiliana na ugaidi.
Kikosi cha bendi ya jeshi la anga la kenya kabla ya kuwasili kwa Rais wa Marekani, Barack Obama kwenye ikulu mjini Nairobi, Jumamosi, July 25, 2015. Rais Obama amelitaja bara la Afrika linasonga mbele, akiwa nchini Kenya Jumamosi, katika taifa la Afrika Mashariki ambalo ana uhusiano nalo mkubwa wa kifamilia.
Msichana Joan Wamaitha mwenye umri wa miaka nane, akimlaki Rais Barack Obama kwa maua alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kenyatta, Ijumaa, Julai 24, 2015, huko Nairobi, kenya. Obama ni rais wa kwanza wa Marekani aliyepo madarakani kuitembelea Kenya, sehemu ambako baba yake amezaliwa.
Rais Barack Obama anashiriki katika mkutano wa pamoja na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta huko Ikulu, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi, Kenya.
Rais Barack Obama, kulia, akipeana mikono na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kabla ya mkutano wa pamoja huko Ikuly, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi, Kenya.
Rais Barack Obama akiangalia baada ya kuweka shada la maua, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi, kwenye Memorial Park kuwakumbuka waathirika wa mashambulizi ya mabomu ya mwaka 1998 kwenye ubalozi wa marekani.
Rais Barack Obama, kulia, anapeana mikono na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kabla ya kuhutubia kwenye mkutano wa kimataifa wa wajasiriamali, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi.
Rais Barack Obama, kushoto, akishiriki katika majadiliano kwenye mkutnao wa Global Entreprenuership Summit uliofanyika katika jengo la Umoja wa Mataifa, Jumamosi, Julai 25, 2015.
Rais Barack Obama akishiriki katika sherehe za kuweka shada la maua, Jumamosi, Julai 25, 2015, mjini Nairobi, kwenye Memorial Park kuwakumbuka waathirika wa mashambulizi ya mabomu ya mwaka 1998 kwenye ubalozi wa Marekani.
Rais wa Marekani, Barack Obama analakiwa na rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, kulia, alipowasili Ikulu mjini Nairobi, Jumamosi, Julai 25, 2015.