Papa Francis ameunda jopo maalum ili kutathmini nafasi ya mwanamke msaidizi wa padre katika kanisa katoliki.
“Baada ya sala za hali ya juu na kufanya taamuli Papa ameamua kuunda tume hiyo ya kutathmini nafasi ya usaidizi wa mwanamke kwa padre, ofisi ya Vatikan ilieleza katika taarifa.
Papa alimteuwa askofu Luis Fransisco Ferrer katibu wa muungano wa waumini wa imani ya kanisa kama rais wa 13 wa tume. Pia wanawake 6 na wanaume 6 kutokamtaasisi za elimu duniani wataumikia katika tume hiyo taarifa hiyo ilieleza.
Vatikan haikuweka siku maalum kwa tume hiyo kuanza kazi siku ya tamatai kufikia ukamilisho.