Your browser doesn’t support HTML5
Papa Francis anatarajiwa kuwasili jamhuri ya afrika ya kati jumapili, ilikwa ni kituo cha mwisho cha ziara yake barani Afrika. Taifa hilo limekumbwa na mizozo tangu mapinduzi yalofanywa na waasi mwaka 2013 na kupelekea ghasia miongoni mwa jamii za kiislamu dhidi ya jamii za wakristo. Wengi wanataraji papa ataweza kuleta Amani nchini humo.
Msikiti katika mtaa wa PK5 mjini Bangui, unajitaarisha kwa ziara ya papa Francis. Takriban miaka miwili baada ya maelfu ya waislamu wa Bangui walipokimbia mashambulizi yalofanywa na magenge na wanamgambo. Hali imebadilika kidogo tu. Waislamu waliowa chache walobakia au walorudi huko PK5, wanasema wanahofia maisha yako iwapo watoondoka eneo hilo.
Papa Francis anatarajiwa kuhotubia ujumbe wa amani kwa waislamu na wakristo huko jamhuri ya Afrika ya kati.
Oumar Kobine Layama ni rais wa baraza la waislamu nchini humo. Amefanya kazi kuleta maridhiano.
Oumaru anasema, tunamatumaini kwamba ziara ya papa itaweza kuleta mabadiliko makubwa kwa mioyo ya watu wa jamhuri ya afrika ya kati, ambayo itapelekea kurejea Amani na kurejea kwa waislamu na wakristo kuishi pamoja. Hili litapelekea maendeleo ya taifa.
Jamhuri ya Afrika ya kati ilitumbukia kattika ghasia mwaka 2013 baada ya waasi wa Seleka kuchukuwa madaraka. Vita vya kulipiza kisasi viliibuka baadae mwaka huo, pale wanamgambo waliposimama na waasi wengi wa kiislamu kutoondolewa madarakani.
Mapigano yameuwa maelfu ya watu. Maelfu wengine wametoroka nchi au kuhamia kwenye kambi kama hii katika kanisa la kikatoliki mjini Bangui.
Walinda Amani wa umoja mataifa wanalinda kanisa ambapo papa Francis anatarajiwa kufanya ibada.
Wengine wanasema mambo ni magumu kidogo.
Bangui imekuwa shwari katika siku kupelekea kuwasili kwa papa. Lakini kila mahali nchini, ghasia zinaendelea. Mapigano mapema mwezi huu, yaliuwa watu 22 huko maeneo ya mashambani.