Pompeo anasisitiza sera za Trump kwa Iran

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo, April 29, 2018.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, yupo Israel kwa ziara yake ya kwanza ya kanda ya mashariki ya kati tangu alipoidhinishwa kuchukua wadhifa huu mpya.

Aliwasili Jumapili akitokea Saudi Arabia, ambako mshauri mwandamizi wa sera wa Pompeo, Brian Hook anaefuatana naye, alitoa wito kwa washirika wa ulaya na nchi nyingine kuweka vikwazo kwa Iran ili kupunguza nguvu za program yake ya makombora. Hook aliwaambia waandishi wa habari huko Riyadh kwa maneno yake “tunayasihi mataifa kote duniani kuwawekea vikwazo watu na viongozi wenye uhusiano na program za makombora za Iran, akiongezea kusema hilo lilikua suala kuu kwenye majadiliano yake na mataifa ya ulaya.

Ziara ya Pompeo huko mashariki ya kati inatarajia kuwaelezea washirika wa Marekani juu ya sera za utawala wa Rais Trump kuelekea Iran na baadae kurejea nyumbani mjini Washington DC.