Mohammed al- Zarqa msemaji wa jeshi la polisi amesema “ polisi wa palestina waliandaa mpango ambao utajumuisha vitengo vyote vya jeshi la polisi.
Mpango huu una lengo la kuimarisha ulinzi na uthabiti na kuanza tena vituo vya polisi katika maeneo ambayo watu wanaweza kufikika kwa urahisi .
Makubaliano yalifikiwa Jumapili baada ya vita vya miezi 15 kwa kubadilishana mateka wa kwanza watatu waliokuwa wanashikiliwa na Hamas na kuachiliwa kwa wapalestina 90 kutoka jela za Israel.
Sasa mwelekeo ni kuanza kujenga tena ukanda huo ambao jeshi la Israel limeharibu na kuwa vifusi vingi katika kampeni zake za kutaka kuangamiza kundi la Hamas ikilipiza kisasi cha shambulizi la Octoba 7 la mwaka 2023 dhidi ya Israel.