Vituo hivyo ni KTN News, Citizen, NTV, Inooro TV and Radio Citizen vimesitisha matangazo yake kufuatia hatua ya Mamlaka ya Mawasiliano nchini Kenya kuvinyang’anya uhuru wao wa kutupa matangazo kwa umma.
Wanaharakati hao walikuwa wanaandamana kuelekea ofisi za serikali katikati ya Jiji la Nairobi ndipo polisi walipotupa mabomu hayo ya machozi.
Vyanzo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa serikali bila kujali imeendelea kuvifungia vituo hivyo pamoja na kuwa mahakama imeamuru kuwa serikali iondoe katazo la vituo hivyo kupeperusha matangazo.
Maandamano hayo yalihusisha makundi ya kutetea haki za kibinadamu, waandishi wa habari na baadhi ya wananchi walioandaman Nairobi kuishinikiza serikali kutii amri ya mahakama.
Siku ya Ijumaa mwanaharakati Okiya Omtatah amedai kuwa polisi walimzuia kuingia katika jengo la makao makuu ya mamlaka ya mawasiliano jijini Nairobi ambako alikuwa anakwenda kupeleka amri ya mahakama iliyokuwa inaondosha marufuku ya matangazo iliotolewa kwa vyombo vya habari.