Polisi kuendelea kudhibiti "mtandao" wa mashoga Tanzania

Maandamano nchini Malawi yakupinga kifungo kilichotolewa kwa mtu aliyekuwa anadaiwa kujihusisha na ushoga nchini Malawi, 2010.

Watu 12, wakiwemo wananchi wawili wa Afrika Kusini na mwananchi wa Uganda wamekamatwa na polisi wakidaiwa kuwa ni mashoga, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya serikali ya Tanzania katika kupambana na ushoga.

“Tumewakamata wahalifu hawa katika hoteli ya Peacock—wakiwa wanaufagilia ushoga. Wawili kati yao ni wananchi wa Afrika Kusini, mmoja ni Mganda na tisa ni Watanzania,” mkuu wa polisi Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amesema.

Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimesema Kamanda huyo amesema kuwa wengine 12 bado wanahojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani na hakusema ni lini walikamatwa.

“Sheria za Tanzania zinakataza kitendo cha mapenzi kati ya watu wa jinsia moja na ni uvunjifu wa sheria za nchi,” amesema Mambosasa.

Ameongeza kuwa meneja wa hoteli hiyo ni miongoni mwa watu waliokamatwa “kwa kuwapa chumba” watu hao.

Mombasa amewahimiza watu kutoa taarifa kwa vyombo vya umma iwapo watakuwa wameshuhudia harakati kama hizo "ilituweze kuchukua hatua mara moja".

Polisi pia wamewakamata watu 20 kati yao wanane ni wanaume na 12 wanawake kwa makosa ya ushoga katika kisiwa cha Zanzibar mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa polisi, zoezi la kuwakamata lilifanyika katika hoteli ambako kikundi hicho kilikuwa kinapewa mafunzo na Asasi ya kiraia ya kimataifa iliyokuwa imesajiliwa rasmi, inayojihusisha na elimu juu ya ukimwi.

Mwezi Februari, Tanzania ilikosolewa na Marekani baada ya kutangaza kufunga vituo vya afya kadhaa vinavyoshughulikia kuelimisha watu kujilinda na Ukimwi, ikidai kuwa vilikuwa ni vituo vya kuhamasisha ushoga.

Serikali Dar es Salaam iliahidi kuwaondoa nchini raia wa kigeni wote wanaofanya kampeni kutaka mashoga wapewe haki zao.

Ushoga kwa kukutana kimwili wanaume unaadhibiwa kwa kifungo kati ya miaka 30 hadi maisha katika Sheria za Tanzania. Hakuna katazo kama hilo kwa kosa la mapenzi baina ya wanawake.

Kwa mujibu wa Shirika la Haki za Binadamu Amesty International, ushoga ni kinyume cha sheria katika nchi 38 kati ya nchi za Kiafrika 54 na adhabu yake ni kifo huko Mauritania, Somalia na Sudan.
Uganda in 2014 tried to impose the death penalty on those found guilty of being homosexual, however the controversial law was later repealed.

Uganda mwaka 2014 ilijaribu kuweka adhabu ya kifo kwa wale watakao kutinakana na kosa la kujihusisha na ushoga , lakini sheria hiyo tata iliondolewa kabisa siku za usoni.