Ni mwandishi wa vitabu wa pili kukamatwa na maafisa katika miezi ya karibuni.
Tumuhimbise ambaye anaongoza kundi la shinikizo la ndani ya nchi, The Alternative Movement na chombo cha habari cha mtandaoni, Alternative Digital, alikuwa anatarajiwa kuzindua kitabu cha kumkosoa rais Yoweri Museveni tarehe 30 Machi.
Inasemekana Tumuhimbise na wenzake walikamatwa na kuwekwa ndani ya gari na maafisa wa usalama waliokuwa na silaha Alhamisi iliyopita.
Msemaji wa polisi, Fred Enanga ameliambia shirika la habari la AFP kwamba “ Polisi walipata malalamiko kuwa kundi hilo lilihusika katika mawasiliano ya kuudhi na kutangaza matamshi ya chuki”.
Wakili wa washukiwa hao, Eron Kiiza aliiomba mahakama ya mjini Kampala iwaachilie huru jana Jumatatu, akidai kuwa polisi walichukuwa simu, laptop, kinasa sauti na kamera za chombo cha habari cha Tumuhimbise.