Polisi wa Uganda wamewakamata watu wengine watano na kugundua vilipuzi vingine vitano karibu na mji mkuu Kampala katika njama ya kulipua mabomu inayohusishwa na kundi la waasi wa Kiislamu, jeshi hilo lilisema.
Wakiwa na makao yao katika misitu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Vikosi vya Allied Democratic Forces (ADF) vinaungana na vuguvugu la wanamgambo wa Islamic State na kwa miaka mingi wameshambulia raia na maeneo ya kijeshi nchini Congo na Uganda.
Mamlaka nchini Uganda ilimkamata mshukiwa wa kwanza akiwa na bomu kwenye begi nje ya kanisa moja lililojaa siku ya Jumapili, na kusababisha msako ambao ulipelekea kukamatwa kwa watu wengine watano na kupatikana kwa vilipuzi vingine vitano, polisi walisema.
Mabomu hayo yaliteguliwa kwa usalama na vitu vikiwemo misumari, betri na vifaa vya kulipua vilipatikana, polisi walisema katika taarifa Jumatatu jioni.