Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mjini Nairobi na mamlaka hiyo, maafisa sita wa polisi watashtakiwa kwa makosa ya mauaji na unyanyasaji, baadhi wakituhumiwa kuhusika kwa vitendo vya kufyatua risasi kiholela dhidi ya raia wakati wakitekeleza masharti ya marufuku hiyo.
Polisi pia wanatuhumiwa kwa kutumia nguvu kupita kiasi badala ya kutii sheria wakati wakitekeleza majukumu yao.
Nalo shirika la umoja wa mataifa la kutetea haki za binadamu, pia linawashutumu polisi wa Kenya kwa makosa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mauaji na unyanayasaji wa kingono kwa baadhi ya raia.
Hata hivyo, idara ya polisi imesema matukio yatanayotajwa katika ripoti hizo, yanatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa kina.
Tangu masharti mbalimbali kuwekwa na serikali ya Rais Uhuru Kenyatta katika juhudi za kupambana na ugonjwa huo wa Corona, Wakenya katika miji mbalimbali wamekuwa wakilalamikia hulka ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi, na kuwanyanyasa kwa njia mbalimbali.