Polisi wa Kenya wakamata watu wawili kuhusiana na mauaji ya mwanariadha wa Uganda

Hayati Benjamin Kiplagat wa Uganda aliposhiriki mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji kwa wanaume katika mashindano ya riadha wakati wa Michezo ya Olimpiki ya London 2012 Agosti 3, 2012 mjini London.

Polisi wa Kenya wamesema wamewakamata watu wawili leo Jumatatu kuhusiana na mauaji yaliyotokea mwishoni mwa juma ya mwanariadha wa Uganda .

Watu hao wawili wanaoaminika kuwa katika umri wa miaka 30 walikamatwa katika viunga vya Rift Valley kwenye mji wa Eldoret, kamanda wa polisi wa eneo hilo Stephen Okal alisema.

Washukiwa hao wawili ni wahalifu wanaojulikana kwakuwatishia kuutishia umma, Okal aliambia AFP.

Tuko katika hatua ya juu ya upelelezi na labda tutawapeleka mahakamani kesho.

Kiplagat mzaliwa wa Kenya alikuwa ameiwakilisha Uganda kimataifa katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi, ikiwa ni pamoja na katika Michezo kadhaa ya Olimpiki na Mashindano ya Dunia.