Polisi wa Israel wazingira nyumba ya aliyefanya shambulizi Israel

Polisi wa Israel, Jumapili waliizingira nyumba ya familia ya Mpalestina aliyefanya shambulizi siku mbili zilizopita na kuua watu saba nje ya nyumba ya ibada.

Tukio limetokea wakati hofu zikiongezeka baada ya miaka kadhaa ya kutokuwepo uthabiti Jerusalem, na ukingo wa magharibi.

Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ametangaza mipango ya kufanya iwe rahisi kwa Waisrael kubeba bunduki baada ya shambulizi hilo baya dhidi ya Wayahudi katika eneo la Jerusalem toka mwaka 2008.

Lilitokea baada ya jeshi la Israek kuvamia kwa miaka kadhaa mji wa ukingo wa magharibi, Jenin. Siku ya Jumamosi kijana wa miaka 13 wa Kipalestina alifyatua risasi kwa kundi la raia wa Israel mjini Jerusalem, na kuwajeruhi kabla ya mmoja wao kumfyatulia risasi na kumjeruhi.